MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 31, 2013

RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA NA NAIBU WAKE LEO IKULU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu, Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.

BONDIA CHEKA AKIMBIA SHULE

                                                     Bondia Francis Cheka akitoka shule.

BONDIA Francis Cheka anadaiwa kukacha masomo katika Shule ya St. Joseph mjini Morogoro alipokuwa anasomeshwa kwa madai ya ugumu wa maisha.

Cheka alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo ikiwa ni ofa baada ya kumtwanga Mmarekani Phill Williams. Mmoja wa walimu wa shule hiyo, James Mkisi amedai Cheka alihudhuria masomo shuleni hapo mara mbili tu!

Cheka amesema kuwa majukumu ya familia pamoja na maisha kuwa magumu ndiyo chanzo cha yeye kukacha shule.

APANDA JUU YA MNARA, ATAKA KUJIRUSHA KWA MADAI YA KUONEWA

 wanausalama wakipanda juu ya mnara kumnusuru jamaa aliyepanda juu ya mnara

Wanausalama wakimshusha jamaa huyo.

 wananchi wakishuhudia tukio hilo

 polisi nao hawakuwa mbali walika mara moja





raia huyo akizungumza na vyo vya habari

Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha. Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kuonewa na polisi.


TASWIRA ZA HAFLA YA KUKABIDHI RASIMU YA PILI YA KATIBA>>> TAZAMA PICHA KIBAO HAPO CHINI