ASKARI polisi mjini Iringa wamefanikiwa kuokoa maisha ya njemba mmoja mkazi wa Ilala mjini Iringa aliyefumaniwa asubuhi ya leo kwa tuhuma za kuvunja amri ya sita na mke wa mtu katika chumba cha wanandoa hao.
Njemba hilo lililofumaniwa limejitambulisha kwa jina na Gilberty Mapunda (35) mzaliwa na Manda wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe ila kwa sasa ni mkazi wa Ilala mjini hapa.
Tukio la kufumaniwa kwa njemba hilo limetokea majira ya saa 12.30 asubuhi ya leo baada ya mume wa mwanamke aliyefumaniwa kufika ghafla eneo la Mkwawa jirani na klabu cha pombe za kienyeji cha Mapinduzi ambako ni nyumbani makazi ya mwanamke huyo .
Hata hivyo katika hali ya kushangaza ni pale njemba hilo kutaka kumshikisha adabu mwenye mke kwa madai kuwa mwanamke huyo alimweleza kuwa hana mume na mume aliyekuwa nae ni ana mke wake hivyo hakuona kosa yeye kumsaidia kumpa huduma mwanamke huyo ambae alikuwa akionyesha kumpenda zaidi .
" Mimi kaka kweli nilidanganywa na mke wako kuwa wewe una mke mwingine hivyo haotafika nyumbani hapo ....lakini naomba unisamehe ama tumalizane kwani tambua kuja kwangu hapo ni kukusaidia kutoa huduma kwa mke wako ambae mimi amenipenda pia"
Pia alisema kuwa kuhusu kuambukizana UKIMWI asiwe hofu ya kumtazama wembamba wake kuwa ni mtu aliyeathirika .
" Kaka naomba unielewe hii afya yangu ya wembamba isikutishe na kunipa adhabu kubwa ukajua nimeathirika hapana hii ni afya yangu ya kawaida .....kama UKIMWI mimi nimetoka kupima juzi tu nipo salama kabisa kwa hilo ondoa shaka"
Mume wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kilave alisema kuwa mke wake anaitwa Beatrice Kisia amepata kuzaa nae wawili akiwemo mmoja wa kike na mwingine wa kiume na hata nyumba hiyo ambayo leo amemfumania mwanaume huyo ni nyumba ambayo ameijenga yeye kwa ajili ya familia yake hiyo .
Alisema kuwa mtuhumiwa wa fumanizi hilo anatambua vema kama mwanamke huyo ni mke wake na kila wakati wamekuwa wakipishana akipeleka huduma .
Kilave alisema kuwa jemba hilo baada ya kuingia katika chumba chake walilazimika kumtoa mtoto mdogo ambae ni mgonjwa na kumpeleka chumba cha pili alichokuwa amelala bibi wa mtoto na wao kuamua kukitumia kitanda hicho kwa mambo yao.
Pia alisema mwanamke baada ya kuona hali ni tete baada ya fumanizi alilazimika kufungua mlango na kukimbia nje na kumuacha mtuhumiwa huyo akiendelea kulala kabla ya kufungiwa katika chumba hicho hadi polisi walipofika na kumchukua .
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kupongeza hatua ya mwanaume huyo kutochukua sheria mkononi .
Mtandao huu wa www.matukiodaima.com umezungumza na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi juu ya tukio hilo na amepata kuthibitisha uwepo wa tukio hilo.
MWISHO