Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi warsha ya siku moja ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar tarehe 9.11.2013.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji wqakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 9 11.2013.
Mke wa RaiS Mama Salma Kikwete akivishwa mavazi ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakati wa warsha ya viongozi wa kimila iliyofanyika Dar tarehe 9.11.2013. Baadaye Mama Salma alipokea zawadi kwa ajili ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete
Olaiboni (CHIFU) wa Kabila la Wamasai Bwana Tikwa Moreto akizungumza na washiriki wa warsha
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Oloiboni Bwana Tikwa Moreto wakati wa warsha
Katibu Mtendaji wa WAMA Bwana Daud Nassib akizungumza na wajumbe wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji hapa nchini iliyofanyika tarehe 9.11.2013.
(PICHA NA JOHN LUKUWI)