Dec 19, 2013
CLEMENT MABINA AZIKWA JIJINI MWANZA
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.