Hapa joel maduka akiwa na Mkurugenzi wa Kwaneema Fm ya jijini Mwanza, akitoa maelezo juu ya Ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi kwa msimu wa Mwaka 2013-2014.
Hapa ni Meneja wa kituo hicho Marium Juma, akitoa maelezo juu ya Tuzo
Frola Jackson,ambae amechukua tuzo ya mfanya kazi bora wa usafi wa 98.2.
Mkurugezi Dinnah Mpemba na mwanadada maarufu kwa jina la spencyoza wakiwa katika pozi wakati wa kupokea tuzo hizo za ushindi mwaka 2014
Joshua Dede,akichekelea baada ya kupokea Tuzo...
The Super Brand Joely Maduka,akipokea tuzo ya mtangazaji anayeongoza kwa kuleta wageni studio kwenye kipindi cha mazingira
picha ya pamoja
wafanyakazi wa kituo cha kwaneema fm radio wakiwa katika picha ya apmoja
Afisa Utawala Msaidizi ambaye pia ni Meneja Vipindi wa Kwaneema Fm Jackline Raphaely akionyesha cheti cha Mfanyakazi bora 2013 alichokipata leo baada ya kuibuka msomaji wa taarifa ya habari bora.
Mmiliki wa Matukio Media Blog Fabian Fanuel (kushoto) akiwa na Mtangazaji wa Kwaneema Fm Joel Maduka
STORY Na:->>>>>
Joel Maduka
Mwanza.Imebainika kuwa kufanya kazi kwa wito pasipo kuweka Maslahi mbele ni silaha ya kushinda hali ngumu ya maisha.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa kituo cha radio ya Kwaneema Pastor Dinnar Mpemba katika hafla za kutunuku tuzo kwa wafanyakazi bora katika Mwaka wa 2013
Akiwataja washindi wa tuzo mbalimbali Meneja wa Kituo hicho Mariam Juma amewapongeza na kuwataka wazidishe bidii katika kazi na kuzidisha ubunifu mwaka huu.
Kwa upande wao baadhi washindi wa tuzo hizo Joel Maduka, Spencioza Haule, Frola John wameelezea hisia zao baada ya kupata tuzo na kuahidi kujituma zaidi kwa mwaka huu mpya ambao anaanza.
Naye Meneja wa vipindi katika kituo hicho Jackline Raphael ambaye ndiye Mshindi wa tuzo ya Mfanyakazi bora ameeleza Siri ya Ushindi wake kuwa ni Mungu na pia kujituma sana katika kazi bila kijihurumia.
Tuzo zilizotolewa ni katika ngazi ya Mfanyakazi bora wa Mwaka mbunifu,Mfanya shughuli kwa kujituma,Mfanyakazi anayejitolea katika kazi ka ziada Mtunza muda na aliyefanya vizuri katika kuleta wageni katika vipindi.