Jan 17, 2014
MWIGULU NCHEMBA AMSHUKIA MBOWE KUWA "MBOWE HAFAI KUWA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGEN
Kumekwepo na jitihada ama za makusudi, ama za kutokujua, ama za kile kinachoitwa kumsafisha mbowe.
Niweke wazi kwamba sikumkosoa mbowe kuhusu mambo ya mahusiano anayosemekana kuwa nayo na wabunge wake wa viti maalumu, bali ni kuhusu KUKIUKA KWAKE MAADILI YA UONGOZI.
1) Kitendo cha kukatisha ziara ya mbunge wake wa kazi maalumu ili wakakutane Dubai kwa kazi maalumu badala ya kazi ya nchi aliyotumwa tena arudi toka marekani mpk Dubai kwa fedha za serikali ni matumizi mabaya ya
fedha za umma na ni ukosefu wa maadili ya uongozi. Angemrudisha kwa gharama zake yaani kwa fedha zake hapo ingekuwa mambo binafsi. Kufanya mambo binafsi kwa fedha ya umma haiwezi ikawa jambo binfsi. Hivyo sikukosoa mapenzi yao bali matumizi ya kodi za masikini kwa mambo binafsi.
2) Kumlazimisha Afisa wa bunge abadili tiketi ileile iliyokuwa aende kwenye shughuli ya bunge sasa ageuze aende kwenye kazi maalumu hili sio jambo binafsi ni matumizi mabaya ya madaraka. Ni kukosa huruma kwa hali ya juu kwa watanzania.
3) Kumlazimisha mbunge wake wa kazi maalumu kuachana na safari ya kikazi na kuacha nchi ikose mwakilishi kwenye kikao hicho huku tayari akuwa ameshagharamiwa safari hiyo, huku tayari akiwa ameshaziba fursa hiyo ambaye mbunge mwingine angeweza kwenda kuliwakilisha taifa halafu mbowe na mtu wake wakaenda kwenye kipaombele chake cha kuburudika dubai ni ukosefu wa uzalendo kwa Taifa na ni ukosefu wa maadili ya kiuongozi.
Tumeongea kwakuwa wametumia fedha za umma, tumesema kwa sababu wameacha kazi ya umma huku wakiwa wamechukua fedha kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania na tunasema kwakuwa wamewanyima fursa wabunge wengene ambao wangekwenda kuwakilisha Taifa endapo fursa hiyo hangepewa mtu elibadilishiwa safari ya ya taifa na kuitwa kwa kazi maalumu.
"Ukipewa kazi ya nchi lazima ujiheshimu" NITASHANGAA SANA NITAKAPORUDI BUNGE LIJALO NIKIKUTA MBOWE BADO NI KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI