MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 2, 2014

TIMU YA MADEREVA TAXI IRINGA ''YAIGAGADUA'' 2-1 TIMU YA MADEREVA DALADALA KOMBE LA IRINGA SERVICE STATION

 mchezaji wa timu ya tax akipokea zawadi za ushindi 



 iringa service station

 timu ya tax iringa
 timu ya  Daladala  Iringa

 shabiki wa tax

 Kamanda  wa polisi Iringa Ramadhan Mungi  akitoa  neno  kwa  madereva hao 

 Mratibu  wa mashindano  hayo  kushoto Bw Feisal Abri Asas akifuatilia mashindano hayo  katika  uwanja wa  Samora 


 achana na kitu soka si mchezo mdada amkumbatia kwa kasi ya ajabu mchezaji 
 Ushindi  ulivyowapagaisha mashabiki na wachezaji wa  timu ya Taxi Iringa

 s
 Viongozi  mbali mbali wakiwa  katika meza kuu kabla  ya kukabidhi  zawadi kwa bingwa wa mashindano hayo  kutoka kushoto ni katibu  wa chama cha soka Iringa Ramadhan Mahano , mwenyekiti wa kamati ya  usalama  barabarani  mkoa wa Iringa Salim Abri Asas ,mgeni rasmi kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi,  mjumbe wa  soka  Iringa mzee Mwakasala na Ambwene


 Zawadi  kwa mshindi  wa  nne  timu ya  magari  madodo  jezi ,Tsh 50,000

Mgeni  rasmi  katika mashindano hayo kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa,Ramadhan Mungi akikabidhi  zawadi kwa mshindi wa  pili timu  ya daladala  Iringa


_________________________=============______===============____________

MASHINDANO  ya soka  kwa  ajili ya  kuhamasisha  utii wa  sheria  za usalama  barabarani kwa madereva mjini  Iringa  yamemalizika   kwa  timu ya madereva   Taxi  mjini Iringa  kuibika na ubingwa katika mashindano  hayo.

Mashindano  hayo  yaliyodhaminiwa na kituo cha mafuta  cha Iringa Service Station yalishirikisha  timu  4   za madereva wa  daladala,gari  pick-up,madereva  daladala ,madereva  Taxi na madereva boda boda .

Katika  mchezo  huo   ulioambatana na   hafla ya kuuaga  mwaka  2013 na kuukaribisha   mwaka 2014  na  kupigwa katika  uwanja  wa Samora Iringa ,kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi ndie alipata  kuwa mgeni wa  rasmi katika mchezo  huo ambao ulionyesha  kuwa na mvuto mkubwa  kutokana na timu zote  kuonyesha uwezo wake.

Mbali  ya  timu ya daladala  kufanikiwa  kuonyesha uwezo  wao mkubwa kwa  kuifunga  ngoli la  kufutia machozi kwao  goli  lililofungwa  dakika ya  10  ya mchezo  ila bado  timu ya Taxi  haikukubali  kushindwa katika  mchezo huo.

Hadi  timu  zote  mbili  zinakwenda mapumziko kipindi  cha kwanza  timu ya Taxi ilikuwa haijapata  kuliona  lango la timu ya daladala .

Hata   hivyo  kipindi  cha  pili  kilikuwa na neema  kubwa kwa  timu ya daladala ila bado walishindwa  kutumia vema neema  hiyo  ya magoli  zaidi ya mawili  ya wazi .

Kasoro  kubwa  zilizojionyesha kwa  timu ya daladala ndizo  zilipelekea  timu ya Taxi kujipatia  goli la kwanza  ikiwa ni dakika 65 ya mchezo na  kuongeza goli la pili dakika ya 85 na  kuibuka na ushindi mnono wa goli 2-1

kwa ushindi  huo  timu ya Taxi iliibuka na zawadi  ya jezi  seti  mmoja ,mpira mmoja na Tsh 200,000  wakati  timu ya daladala  ikiambulia jezi  seti moja, mpira  mmoja na Tsh 100,000 huku mshindi wa tatu timu ya boda boda ikipata  seti  ya  jezi ,mpira mmoja na Tsh 100,000 na timu  iliyoshika nafasi ya  nne  timu  ya Pick up  aikipata  seti  ya  jezi ,mpira mmoja na Tsh 50,000

Mratibu  wa  mashindano  hayo Feisal Asas  alisema  kuwa  lengo la kituo  chake  cha Iringa ServiceStation  kuanzisha mashindano  hayo ni  kuamusha hamasa ya michezo kwa   vijana  hasa kwa madereva hao pamoja na  kuwapa  elimu ya usalama  wa barabarani.

Awali mwenyekiti  wa kamati ya usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Salim Asas  alisema  kuwa jitihada mbali mbali zimekuwa  zikifanyika na kamati  hiyo  katika  kutoa  elimu na mafunzo zaidi kwa madereva ili  kupunguza  idadi ya ajali  za  barabarani .

Akizungumza kabla ya kukabidhi  zawadi mgeni rasmi ,kamanda wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa mashindano  hayo  ni chanchu kwa madereva  kujikumbusha sheria za usalama  barabarani.

Kwani  alisema ajali  za barabarani sehemu  kubwa  zinachangiwa na madereva  wasiozingatia  sheria hivyo  iwapo madereva  hawatakuwa makini vifo vya  watanzania  vitokanavyo na ajali  vitaendelea  kuongezeka  zaidi.

Alisema  kuwa takwimu  zinaonyesha  kuwa kati ya mwaka  2012  watu 13  walikufa kwa ajili ya  boda  boda na mwaka 2013 ni  watu 27 wakati  waliojeruiwa  pia  wamezidi  kuongezeka na kuwa sehemu kubwa  ajali  za boda boda zimekuwa nyingi zaidi.

Kamanda Mungi  alipongeza  jitihada za  kamati ya  usalama barabarani  chini ya mwenyekiti  wake Asas kwa kujitolea  kusomesha madereva bodaboda zaidi ya 10000 kwa  kipindi cha miaka miwili  iliyopita.