tundu lissu akiwatuliza wafuasi wa chadema
mwanasheria wa zitto kabwe akiwasili mahakamani
zitto kabwe mahakamani akisikiliza hukumu
tundu lissu akitoka nje ya mahakama baada ya chama chao CHADEMA kushindwa
tundu lissu akizungumza na wananchi kuwatuliza wasiwe na jazba
Stori: Jelard Lucas na Haruni Sanchawa
MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe amekigalagaza chama chake baada ya kuibuka mshindi katika hukumu iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, John Utamwa.
Hukumu hiyo imetolewa leo majira ya saa 11 jioni baada ya Zitto kuwasilisha shauri la kuiomba mahakama iweke zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema (CC) kumjadili kuhusu uanachama wake.
Mahakama Kuu imeamua Zitto aendelee kuwa mwanachama hai wa Chadema mpaka itakamalizika kesi ya awali aliyofungua akidai Chadema kumrejeshea nyazifa zake zote alizovuliwa na chama hicho na kwa kipindi hiki haki zote za mbunge huyo zitakuwa chini ya uangalizi wa mahakama mpaka kesi itakapomalizika na kutolewa hukumu.
Zitto alifungua kesi ya kudai kurejeshewa nyazifa zake ambazo alivuliwa mwishoni mwa mwaka jana, kesi hiyo iliambatana na kesi nyingine aliyoifungua hivi karibuni akiomba Kamati kuu isijadili kuhusu uanachama wake mpaka itakapoisha kesi yake ya awali.
Kesi ya awali yambunge huyo kudai kurejeshewa nyazifa zake itaunguruma tena Februari 13, mwaka huu.