walimu walio hudhuria mafunzo ya ICT wakiwa darasani
walimu wakiwa katika mtihani wa mafunzo ya ICT chuo kikuu huria tawi la mwanza
mkufunzi wa mafunzo ya ICT Bw. Mnyanyi akiwapa elimu walimu waliohudhuria mafunzo ya ICT
wakiwa darasani kwa umakini zaidi wakisikiliza somo kutoka kwa mwalimu wao
wakiwa katika mjadala baada ya mafunzo na hapo aliwauliza swali waliuliza swali
Madam Stella ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari akijibu swali darasani huyu ni muwakilishi toka wilaya ya sengerema ni miongoni mwa walimu waliohudhuria mafunzo ya BASIC ICT SKILLS
wakufunzi wa mafunzo ya Basic ICT Skills wakizungumza na walimu walio hudhuria mafunzo ya ICT
jijini mwanza
mmoja wa walimu aliyehudhuria mafunzo hayo akitunukiwa cheti na wakufunzi wa mafunzo
akiwa na furaha tele baada ya kutunukiwa cheti cha mafunzo ya Basic ICT Skills
wahitimu wa mafunzo ya Basic ICTskills wakionyesha vyeti vyao baada ya kutunukiwa na chuo kikuu huria cha Tanzaia { The open University of Tanzaia}
walimu hao wa shule za sekondari wakionyesha tabasamu na sura zenye kujawa furaha baada ya kuhitimu mafunzo ya BASIC ICT SKILLS
Mwalimu Nestory Ligembe amabye pia nae alipata fursa ya kuzungumza na walimu hao walio hudhuria mafunzo ya Basic ICT skills katika chuo kikuu huria cha Tanzania tawi la mwanza alipata kuongea nao na kuwapa nasaha zaidi juu ya masuala yanayolenga maisha ya Elimu zaidi.
walimu wakiwa katika furaha wakielekea kupiga picha ya pamoja nje ya jengo la PPF PLAZA jijini mwanza ambapo ndipo kilipo chuo kikuu huria cha Tanzania
picha ya pamoja ya walimu waliohudhuria mafunzo ya BASIC ICT SKILLS
kutoka kushoto ni muwakilishi wa walimu waliohudhuria mafunzo na akifatiwa na mratibu wa mafunzo Bw, BENJAMIN BUSSU, akifatia Mwl, Nestor Ligembe, mwisho ni mkufunzi wa mafunzo Bw, Mnyanyi
wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la PPF PLAZA MWANZA
Na wambura Mwikwabe,
Chuo kikuu huria cha tanzania. {The Open University Of Tanzania} kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Tanzania, wametoa kipumbele kwa walimu wa shule za sekondari kitengo cha masomo ya sayansi na hesabu kwa lengo la kukuza mustakabali wa teknolojia ya mwanzo, baadhi ya walimu hapa nchini Tanzania kupitia mpango wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wamepata fursa ya kujiunga na mafunzo yatolewayo na chuo hiki huria cha Tanzania, ambapo mafunzo hayo yamechukua takribani wiki mbili Tangu Tarehe 10 /02/2014 Hadi Trehe 22/02/2014. mkoa wa Mwanzam, kwa kanda ya ziwa wamechukua baadhi ya walimu kutoka baadhi ya wilaya kama vile Geita Bukombe Chato, Sengerema, na pia hata Mkoa kagera pia nao wamepata fursa hii na pia zoezi hili limejuisha mikoa yote ya Tanzania. kwa lengo la kukuza teknolojia na kupeana taarifa zaidi juu ya sayansi na teknolojia haya habari na mwasiliano, hivyo basi baadhi ya wahitmu hao wametunukiwa vyeti vya mafunzo ya BASIC ICT SKILLS.
zoezi hili bado linaendelea katika mikoa mingine kama kawaida.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA CHUO KIKUU HURIA KITENGO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA TAWI LA MWANZA.
THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA
INSTITUTE OF EDUCATION AND MANAGEMENT TECHNOLOGY
MWANZA REGIONAL CENTER
PPF PLAZA TOWER
4th floor and 5th floor
+255756185684/ +255754766910
www.out.ac.tz