MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Feb 13, 2014

IDARA YA UHAMIAJI MBEYA INAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 62 KUTOKA ETHIOPIA

 Wanahabari wakimsikiliza William Bambanganya.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William Bambanganya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jana.

IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya inawashikilia wahamiaji Haramu 62 ambao ni Wahabeshi raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania wawili wakituhumiwa kuingia nchini kinyume na utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William Bambanganya alisema watuhumiwa hao wote wameshafunguliwa mashtaka ya kuingia nchini bila kufuata sheria huku Watanzania wawili wakishtakiwa kwa kuhusika kuwasafirisha wahamiaji haramu.

Alisema wahamiaji hao walikamatwa katika matukio mawili kutokana na kupata taarifa kutoka kwa Watanzania ambao hawapendi vitendo vya kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu kinyume na taratibu hivyo kukiwezesha kikosi cha Uhamiaji kuwatia mbaroni kirahisi.

(Habari/Picha:  Mbeya Yetu)