Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, anaefuata ni Mkurugenzi wa
huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) na watoa huduma wa
duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa
mkoa wa Kagera .
Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akiongea na wananchi na
wanahabari waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba
jana, kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti
nyeusi) pamoja na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka
hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Mkurugenzi
wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (kushoto) akimuelezwa jambo Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani mara baada ya ufunguzi wa duka
jipya la Airtel mkoani Bukoba jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani (kati) akikata keki maalum
iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja Bukoba kwaajili
ya hafla ya kusheherekea ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani hapo.
Wakwanza kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa
Airtel Tanzania Bi Adriana Lyamba na meneja wa duka hilo bukoba bi Anna
Mapunda, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Picha ya pamoja.
======= ====== =========
MKUU
wa Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera Bi. Zipora Pangani ameipongeza
Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel kwa kufungua duka kubwa, ambalo
litatoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo kutuma na kutoa fedha ya
(AIRTEL MONEY).
Akifungua
duka hilo lililopo eneo la Mtaa wa Kawawa Mjini Bukoba, alisema
litakuwani chachu ya maendeleo, kwa wakazi wa mkoani Kagera ambapo
litarahisisha huduma kwa wananachi.
“Ufunguzi
wa hili duka hapa kwetu litakuwa ni chachu ya maendeleo kwa wateja wa
Air tel na wananchi kwa ujumla hasa kwenye matumizi ya huu mfumo wa air
tell money” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu
huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa kagera na maeneo jirani kuhakikisha
kwamba wanaitumia hiyo fursa vizuri ili kuhakikisha wanakuza uchumi wao
katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania alisema ufunguzi wa
duka hilo ni mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine nchi nzima ili
kutoa huduma bora kwa wateja wake.
“
Kampuni yetu ya Airtel tuna mpango madhubuti wakuhakikisha maduka yetu
yote yanakuwa na mwonekano sawa na kutoa huduma bora zenye kiwango cha
hali ya juu kwa wateja wetu kutokana na mahitaji yao” Aliongeza
“
Dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendeana na kasi ya uhutaji kwa wateja
wetu kwenye mawasiliano ya kisasa na teknolojia, ya hali ya juu” Alisema
Mkurugenzi huyo.
Kwa
Upande wao wateja wa kampuni hiyo waliojitambulisha kwa majina ya
Joseph Kamuntu na Eradius Ernest wakizungumza mara baada ya kufunguliwa
kwa duka hilo waliishikuru kampuni hiyo na kwa kuwasogezea huduma hiyo.
“
Tunawashukuru sana hawa watu jamani yaani binafsi nimefurahi sana
kupata hii huduma karibu sasa hivi wamefungua nimeingia mara moja
nimehudumiwa ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine,” Alisema Kamuntu.
Aliyaomba
Mkampuni mengine ya simu kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa
huduma bora ambazo zinamjali mteja ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa
kwa pande zote.
Na. JIACHIE BLOG/WAMBURABABU BLOG