Lori lenye namba za usajili T 158 CSV lililoparamiwa na daladala.
Askari wa usalama wa barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo.
Eneo ambalo daladala hiyo iliyofumuka.
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea.
Lori hilo baada ya ajali.
Hivi ndivyo daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyoharibika baada ya ajali hiyo.
Mashuhuda wakiwa wameizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea.
Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea, askari wa usalama barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo.
Ilikuwa ni ajali mbaya.
Mashuhuda.
Baadhi ya majeruhi wakitolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya.
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na
wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari
mawili.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari
ndogo ya abiria maarufu kama daladala lenye namba za usajili T 237 BFB
aina Toyota Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T
158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea
maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea
Mbalizi kulivaa lori lililokuwa likiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana
na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi ingawa pia walimtupia lawama dereva
wa lori ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi, Mbalizi, Sikitu Mbilinyi,
ambako majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea
majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda Hospitali
ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huku wengine
wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na wanawake wanne na wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana
mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo dereva wa lori
alitokomea mara baada ya tukio.
PICHA / STORI: MBEYA YETU BLOG