MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Aug 31, 2014

Picha: Pastor Myamba azungumzia bajeti ya harusi yake na maisha mapya baada ya kuoa


c
Pastor Myamba akiwa na mke wake Praxceda
Msanii mkongwe wa filamu nchini Emmanuel Myamba, amezungumzia bajeti ya harusi yake iliyodaiwa ilikuwa ya kifahari pamoja na maisha yake mapya baada ya kufunga ndoa. Myamba ambae amefunga ndoa na mwanadada Praxceda huko visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwezi August, ameiambia Blog yetu kuwa
hakutegemea kama ndoa itakuwa kubwa kama ilivyokuwa.
“Namshuru mungu ndoa ilipita salama kama ulivyosikia, unajua budget ya ndoa sikufufichi ilikuwa kubwa ila kusema kwamba ni shilling fulani nitakudanganya, kamati ndo ilikuwa inajua kila kitu ila ndoa ilikuwa kubwa sana, dah kusema kwamba ndoa ilikuwa ya milioni 100 au pungufu nitakuwa sikutendei haki kwa sababu budget sijui ilikuwa kubwa kiasi gani, nawashukuru sana wasanii wengangu ,ndugu, jamaa na marafiki waliyowezesha harusi ikawa kubwa, pia kuna dada yangu ambaye alinizawadia gari na vitu vingine” Alisema Myamba.
Pia Myamba amesema baada ya kuachana na ukapela kuna mambo mengi yamebadilika katika maisha yake.
“Baada ya kuoa najiona mwepesi, unajua maisha ya ubachela yana tabu zake ila sasa hivi nipo safi maisha naona mazuri, kazi zinaenda vizuri, sijawai kuwa na mtoto nazani sasa hivi ndiyo muda muafaka mungu akipenda” Alimalizia Myamba.
                                     Zawadi kutoka kamati ya maandalizi
Zawadi kutoka kamati ya maandalizi
                   Emmanuel Myamba akiwa na mke wake wakati wa kufunga ndoa visiwani Zanzibar
Emmanuel Myamba akiwa na mke wake wakati wa kufunga ndoa huko visiwani Zanzibar

                  a (2)
                  a
d
f
                g
                                   q