Kocha wa England, Roy Hodgson amemteua mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kuwa nahodha mpya wa timu hiyo ya taifa. Rooney mwenye miaka 28 ambae pia ni nahodha ya timu ya Manchester
United, amechukua mikoba iliyoachwa na kiungo wa Liverpool, Steven
Gerrard aliyestaafu.
Rooney aliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha akiiongoza England kwenye
mechi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya San Marino, Oktoba 2012.