Aug 29, 2014
TAHADHARI KWA MAWAKALA WA M-PESA KWA UTAPELI NA WIZI MPYA
Leo mapema blog yetuilipokuwa mtaani katika kusaka habari za hapa na pale ndipo ilibainika kuwepo kwa njia nyingine ya utapeli na wizi wa pesa kwa njia mpya walioibuni matapeli na wezi wa fedha kutoka kwa mawakala. mapema leo Wakala mmoja wa M-PESA maeneo ya kiloleli jijini mwanza ameripot kuibiwa pesa taslimu shilingi elfu sabini T.SH. 70,000/=
wakala huyo wa M-PESA ameiambia blog hii kuwa alikuwa dukani kwake na ndipo alikuja mteja mmoja na kutaka kuwekewa pesa kwenye akaunti yake ya M-PESA alitoa kiasi cha shilingi laki moja na elfu themanini 180,000/= akamkabidhi wakala huyo.
wakati wakala akijiandaa kumpa kitabu cha kusaini malipo ndipo jamaa akageuka na kumwambia samahani naomba kwanza nizihesabu hizo pesa kama ziko sawa ndipo wakala alimkabidhi wakati huo tayari wakala nae alikuwa ameisha zihesabu zikiwa kamili ndipo alipoamua kumpa zile pesa na kuzihesabu kumbe pale pale mteja akauliza kwa makini zaidi kuwa nitajie viwango vya kuweka na kutoa kile kitendo cha wakala kugeuka kutazama karatasi ya viwango vya kutoa na kuweka pesa kwa Akaunti za M-PESA ndipo hapo mteja alipata mwanya wa kupunguza pesa kiasi cha shilingi elfu sabini kisha akamkabidhi wakala zile pesa lakini wakala nae hakuwa makini kukumbuka kuzihesabu tena kama ziko kamili akiwa bado amezishikilia huku akiandika yule mteja alijifanya kuwa na haraka sana ndipoa akaondoka na kupanda ndani ya gari aina ya RAV4.
pale pale wakala akashtuka na kuona pesa ziko pungufu wakati huo mteja kaisha ondoka na ndipo wakala alipoaamua kupiga simu makao makuu ya vodacom kwa WAKALA Mkuu wa M-PESA kila alipokuwa akijaribu kupiga simu simu zikawa hazipokelewi na ndio baadae walipokea wakajaribu kuzirejesha zile pesa ikaonekana tayari zimeisha tolewa kwa wakala mwingine na simu ikawa imezimwa muda huo huo. basi wakala nae akajaribu kuwauliza mawakala wenzake je kama nao walishakumbwa na tatizo la nmana hiyo akapa majibu ya kuridhisha juu ya wizi huo.
Lakini baadhi ya mawakala wa M-PESA AIRTEL MONEY NA TIGO PESA wamekuwa wakilia juu ya wizi wa fedha katika akaunti zao lakini kulingana na mfumo ulivyofanyiwa kazi kwa sasa wizi wa pesa kwa njia za mtandao umepungua kwa kiasi kikubwa sana
Mawakala hoa wameripoti kuwa wizi uliobakia ni ule wa mteja anakuja na pesa anakukabidhi kisha anakuomba pesa tena azihakiki kama ziko sawa na kupunguza kiasi cha fedha, lakini pia kumekuwa na wizi wa kutumia madawa ya mazingaombwe ni pale tu mteja anapokuja na pesa kisha anakuomba tena zile pesa ukimrudishia tu anaweka pesa za kuibia palepale atakapo ondoka tu na pesa ulizokabidhiwa nazo hazionekani sasa Mawakala jijini mwanza wameanza kuwa makini sana kwa wizi wa namna hiyo kwani imekuwa ni changamoto sana kwao katika biashara hiyo
ya KUTUMA NA KUPOKEA PESA
TAHADHARI KWA MAWAKALA
1. usitume pesa nje ya mteja anae hitaji huduma papohapo kwa kudanganywa kuwa naomba umtumie mtu pesa yuko mahari fulani hiyo itakula kwako fuata maelekezo ya Wakala mkuu namna ya kutma na kupokea pesa nje ya area yako.
2. unapopokea pesa hakiksha umezihesabu kwa makini sana na usimrudushie mteja pindi atakapo zihitaji tena kwani zaweza zisirudi zote zikiwa kamili
.
3. hakikisha mteja anaweka sahihi yake kwenye daftari la wakala wa M-PESA kabla ya kuondoka mahali hapo ulipo
4. Ripoti haraka kwa huduma wa wateja au kituo cha polisi ili kudhibiti uhalifu na wizi wa utapeli juu ya M-pesa
5. Hakikisha hakuna mtu yeyote anae itambua namba yako ya siri ya M-PESA kwani waweza kuibiwa pesa zote katika akaunti yako ya M-PESA