Serengeti fiesta Moshi wapewa fursa ya kuonja radha
Mhehimiwa
Temba ametangaza rasmi kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la
"Wazee wa jiji" jumamosi hii. Serengeti fiesta Moshi wamepewa fursa ya
kuonja radha ya wimbo huo siku ya Jumamosi katika uwanja Majengo Jijini
humo.
Mheshimiwa
Temba ambaye ni mzawa wa
jiji hilo anatarajia kutumia fura ya Serengeti fiesta Moshi kuuzindua wimbo huo kwa mara ya kwanza.
jiji hilo anatarajia kutumia fura ya Serengeti fiesta Moshi kuuzindua wimbo huo kwa mara ya kwanza.
"Ni
matumaini yangu kuwa Wanamoshi wataniunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi
katika viwanja wa Manjengo siku ya Jumamosi Agosti 30, kushuhudia shoo
kali nitakayoifanya sanjari na nyota wengine wa muziki watakaotumbuiza
katika tamasha hilo.
Baadhi ya
wasanii watakaowasha moto katika jukwaa la Serengeti fiesta Moshi ni
pamoja na Ali kiba, Ney waMitego, Dully Sykes, Jambo Squad, Stamina,
Maua, Recho, Shaa and Mapacha, Chege na Temba na wengine wengi.
Chege
ameishukuru kampuni ya Serebgeti kupitia kinyaji chake mashuhuri,
Serengeti Premium Lager, kwa kutoa fursa kwa wasanii kukutana na
mashabiki zao na kuwapa burudani. "Burudani la Serengeti fiesta ni moja
ya mifano dhahiri inayoonyesha jinsi Watanzania tunavyopendana bila
kujali utofauti wa makabila yetu na dini zetu."(Martha Magessa)
Temba
ameyashauri makampuni mengine yanayopatikana ukanda wa Afrika Mashariki
na kati kuiga mfano wa Serengeti Fiesta ili kudumisha udugu na ujamaa
katika nchi wanazofanya kazi.
Pia
ameishauri kampuni ya Serengeti fiesta kuangalia uwezekano wa
kulisambaza burudani hili katika nchi nyingine Africa...ikianzia na
Afrika ya Mashariki.
"Burudani
inanguvu ya kipekee sana katika maisha ya manadamu. Kwa kuisambaza
Serengeti fiesta katika nchi nyingine Afrika mashariki kutaifanya jumuia
hii kuungana zaidi na kuwa kitu kimoja," alisema Temba.
Baada ya
Mohi, Burudani la Serengeti fiesta litaelekea mikoa mingine kama Musoma,
Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Moshi, Arusha, Mtwara na
baadae jijini Dar es salaam.