Afisa Vijana wa UMATI kutoka Temeke Bibi. Upendo Daud akimkabidhi
zawadi ya machapisho kuhusu Afya ya uzazi wa mpango Mwenyekiti wa Mtaa
wa Sabasaba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika Jamvi la Vijana
lililofanyika katika mtaa wake. Jamvi la Vijana ni program ambayo
inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya
Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki
ya juu ya uzazi wa mpango?”Baadhi
ya wakazi wa mtaa wa Sabasaba wakipata maelezo kuhusu afya ya uzazi wa
mpango kutoka kwa waelimisha rika wa UMATI walipokuwa katika Jamvi la
Vijana lilioshirikisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka Manispaa
ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni.Mmoja
wa washereheshaji katika Jamvi la Vijana akimkabidhi mtoto Shani Rajab
zawadi ya Jarida la Fema baada ya kujibu swali kuhusu uzazi wa mpango
katika Jamvi la Vijana lililofanyika katika mtaa wa Sabasaba na
kuhusisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka kata ya Mtoni
iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni.
Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo
cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana
limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?” Baadhi
ya wananchi wakifuatilia igizo kutoka kwa Kikundi cha Vijana cha Benki
Club (hakipo pichani) wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika mapema
hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni
Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni program
ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka
Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya
“Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?” Baadhi
ya waigizaji wa Kikundi cha Vijana cha Benki Club wakiigiza kuhusu
namna ambavyo mwanaume anamshinikiza mke wake abebe mimba mara baada
ya miezi michache tokea ajifungue,igizo hilo lilionyeshwa wakati wa
Jamvi la Vijana lililofanyika mapema hivi karibuni katika mtaa wa
Sabasaba kata ya Mtoni iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia
Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana
limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?” Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni Manispaa
ya Temeke jijini Dar es Salaam Bw. Ibrahim Mwita (waliosimama
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kikundi cha Vijana
cha Benki Club wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika jijini Dar es
Salaam mapema hivi karibuni. Picha zote na Frank Shija, MAELEZO