Kipa
wa Ujerumani na Bayern Munich Manuel Neuer Mshambulizi wa Uholanzi
Arjen Robben wamejiunga na mshindi wa tuzo la mchezaji bora duniani
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ni miongoni mwa wachezaji wanaowania
taji la mchezaji bora barani Ulaya.
Watatu hao walichaguliwa na waandishi wa habari za michezo kufuatia utendakazi wao uwanjani katika msimu wa mwaka wa 2013-2014.
Nuer alikuwa ngao ya mabingwa wapya wa dunia Ujerumani huku Robben akitikisa wavu mara 21 .
Kwa
upande wake mchezaji bora duniani mwaka huu Christiano Ronaldo alifunga
mabao 17 msimu huu na kuiongoza Real Madrid Kutwaa taji la mabingwa
barani Ulaya.
Mshindi atatuzwa katika hafla ya kutangaza droo ya mwaka huu ya kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya huko Monaco.
Wachezaji kumi waliteuliwa kulingana na wingi wa pointi waliozojizolea .
Wengine katika Orodha hiyo ni Thomas Muller (Bayern Munich, ) 39 ; Philipp Lahm (Bayern Munich, ) 24, Lionel Messi (Barcelona, Argentina) 24; James Rodriguez (Monaco/Real Madrid, Colombia) 16; Luis Suarez (Liverpool/Barcelona, Uruguay) 13; Angel Di Maria (Real Madrid, Argentina) 12; Diego Costa (Atletico Madrid/Chelsea, Uhispania ) 8