WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Ujenzi
wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF
imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa
daraja hilo.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi
unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana
na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari
kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.
Alisema kuwa juhudi za NSSF katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo
unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa
barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.
Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads.
Msafara
wa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ukiwa katika ukaguzi wa
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali.
Waziri
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akipata maelezo ya
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka kwa Meneja wa Mradi wa
ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Kareem Mataka, wakati alipofanya ziara
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.
Mh. Magufuli akifafanua akitoa maelekezo kwa Mhandisi Kareem Mataka (kulia).
Wavuvi wakivua samaki katika eneo la mradi wa ujenzi wa daraja hilo.
Mhandisi
wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka akitoa maelezo
ya maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo kwa Waziri wa Ujenzi John
Magufuli alipofanya ziara kujionea maendeleo ya daraja hilo.
Waziri
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akikagua maendeleo ya
ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali. Kulia ni Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka.
Waziri akiwa katika zira ya ukaguzi pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Ujenzi, NSSF pamoja na waandishi wa habari.
Ukaguzi wa Daraja.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick
Mrosso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Miradi wa NSSF, Yakub Kidula.
Waziri
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kulia), akimpongeza Meneja Mradi ujenzi
wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka mara baada ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa daraja hilo.
Waziri
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akimshukuru Kaimu Mkurugenzi wa NSSF,
Ludovick Mrosso kutokana na kazi nzuri inayofanywa na NSSF katika ujenzi
wa daraja la Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akibadilishana mawazo na Meneja wa Mradi
wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka, Mkurugenzi wa Miradi wa NSSF,
Yakub Kidula (katikati), baada ya kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa
daraja la Kigamboni.