Mkurugenzi
wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, (Wa pili toka Kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea
uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya
Alhamis Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club. Pembeni yake
ni Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere na wasanii wengine
FILAMU
ya ‘Mateso Ughaibuni’ ambayo imerekodiwa Uingereza na wasanii Issa
Musa ‘Cloud 112’, Riyama Ally, Wastara Juma na Monalisa itazinduliwa
Alhamisi hii katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Didas
Fashion, Khadija Ayoub Seif, ambaye kampuni yake ndiyo iliwapeleka
wasanii hao Uingereza kwenda kurekodi filamu hiyo, alisema licha ya
kampuni yake kujihusisha na mambo ya mavazi na vitu vingine ameona kuna
kila sababu ya kuwasaidia Watanzania wanaofanya sanaa ya uigizaji.
Rais
wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea machache mbele ya waandishi wa
habari juu ya uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni. Pembeni yake ni
Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif na Flora Mvungi.
Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini.
Wafanyakazi wa PSPF nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
picha na habari kwa hisani ya Kajunason Blog/wamburababu