Mkuu wa shule ya sekondari ya Ifunda Tech akizungumza na wanafunzi hao hivi karibuni
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ifunda Tech
Uongozi
wa shule ya sekondari ya Ifunda tech wilaya Iringa mkoani Iringa
imewaita wanafunzi 28 kufika shuleni hapo octoba 2 ikiwa ni baada ya
shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana kutokana na wanafunzi hao
kufanya vurugu kubwa hivi karibuni.(P.T)
Hatua ya
uongozi wa shule hiyo kuwaita wanafunzi hao imekuja zikiwa ni zaidi ya
siku 4 kupita toka shule hiyo kufungwa kufuatia vurugu kubwa shuleni
hapo na kusababisha hasara kubwa ya mali za shule hiyo Makamu mkuu wa shule hiyo Ernest Sakafu ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na mtandao wa matukio daima ofisini kwake .
Amewataja
wanafunzi wanaotakuwa kufika shuleni hapo kuwa ni steven Nyiriri,petro
Kalolo,Iddi shaban,John Zephania,Edwin Rwegoshora,Adinan mrisho mtiti
,Izengo Dotto,Gaspar Manyagi,shemson Amoni ,Halid Omari,said sambo
,paschal lusukanija ,Fred Kidava na Eliji Nguvila Wengine
ni Stambuli Daluweshi,Jackson Mlowe,Sidi Kayombo,Yusuph Makale , Joseph
Antony ,Allan Laurent , Rose Kayombo,Enoce John ,Rashid Kandoro ,Abdul
Zumo ,Petro Silwimba ,Joyce Nestory ,Michael Kimario na Athuman Ahamad Alisema kuwa kwa sasa shule hiyo imefungwa kutokana na vurugu hizo hivyo shule hiyo itafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa