MSANII wa siku nyingi katika tansia ya filamu Bongo, Salama Salmin
‘Sandra’ amefunguka kuwa tangu ameanza kujihusisha na mambo ya sanaa
hajawahi kuwa na bwana ndani ya klabu ya Bongo Movies na wala hajawahi
kutoa rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ kama ilivyo kwa wengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Sandra alisema
kuna baadhi ya wasanii wanafikiri kuwa na mwanaume ndani ya Klabu ya
Bongo Movie ndiyo kutimiza ndoto zao kumbe ni kujidharaulisha tu.
“Sina bwana wala sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ na
sifikirii kufanya hivyo kamwe, maana ni kujishushia heshima yangu
wakati mimi ni mke wa mtu na wala siwezi kunadi mwili wangu,” alisema
Sandra.