1.KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA RS MWANZA.
DANNY TEMBA, AKIMSIKILIZA KATIBU MKUU UTUMISHI WAKATI WA KIKAO NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA HIVI LEO.
PATRICK KIGERE, AFISA MANUNUZI SKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA AKITOA MOJA YA KERO ZINAZO WAKABILI.
KIKAO CHA KATIBU MKUU UTUMISHI NA WAFANYAKAZI KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA.
KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA.
KATIBU MKUU
UTUMISHI GEORGE YAMBESHI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA
SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA. (PICHA NA AFISA HABARI WA RS MWANZA)
---
Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa
Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria,
kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.
Ameyasema hayo
wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye
ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo
kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na
watumishi hao.
Yambeshi amesema
kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi
wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo
na utata kwa watu " kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo
tuongoza" alisema na kuongeza. kuwa suala la kuvujisha siri za serikali
ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni
lazima ajue kutunza siri.
Katika hatua
nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo
ya siasa mahali pa kazi" Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama
cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa
kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa
umma.
Mbali na masuala
la siasa na uadilifu katika kazi ,pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa
hiyo, kusilikiliza kero mbali mbali za watumishi hao ikiwapo suala la
kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya
miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.
Awali
akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa
Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza
Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi
katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu
ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala
wa serikali na wale wa serikali kuu.
Hata hivyo
katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto
zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri
itakavyowezekana.