Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa
Warsha ya siku mbili ya Waandishi wa Habari ilinayoendeshwa na Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya
hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa
umma,inayofanyika kwenye hoteli ya Oasis mjini Morogoro.Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na
kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
nchini,Dkt. Hamza Kabelwa.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya
Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu
umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa
taarifa za hali ya hewa kwa umma wakisikiliza kwa makini hotuba ya
ufunguzi wa warsha hiyo iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro,Mh. Joel Bendera.
Mkurugenzi
wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza
Kabelwa akizungumza machache wakati akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na
kwa washiriki wa warsha hiyo inayoendelea kufanyika hivi sasa kwenye
ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt.
Hamza Kabelwa akizungumza jambo wakati akichangia moja ya mada
zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo inayoendelea hivi sasa
kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi akisisitiza
jambo wakati akijubu moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari
wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,inayohusu umuhimu wa huduma za hali ya
hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma
Muwasilishaji
wa Mada ya kwanza katika warsha hiyo,Bi. Mecklina Merchades
akiwasilisha mada iliyohusu Utekelezaji wa programu ya utoaji huduma ya
hali ya hewa duniani.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na Mkurugenzi
wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza
Kabelwa wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada mbali mbali
zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya
Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu
umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa
taarifa za hali ya hewa kwa umma wakifatilia kwa makini mada
zinazoendelea kutolewa kwenye warsha hiyo.
Picha ya pamoja.