|
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi nahodha wa
Mkolani Fc Meck Lyimo, kombe la ubingwa wa Michuano ya Pepsi Kombe la
Meya 2014 mara baada ya timu hiyo kuifunga timu ya kata ya Mirongo bao
2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jumamosi uwanja wa Nyamagana
jijini Mwanza na kuhudhuriwa na mashabiki wengi. |
BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJIRI.
|
Kikosi
cha timu mabingwa Mkolani Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na
Mirongo Fc kwenye mchezo wa fainali Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa
kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. |
|
Kikosi
cha timu Mirongo Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na Mkolani
Fc kwenye mchezo wa fainali Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. |
|
Ni
wakati wa kupata mawaidha toka meza kuu ya wageni na wenyeji wa
Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ambayo mwasisi wake ni Mstahiki
meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula. |
|
Balozi
wa habari wa Pepsi Albert G. Sengo (katikati) akitoa utangulizi
kuhusiana na Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, mbele ya meza kuu.
|
|
Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa,
(mbele) akiongoza msafara wa Meza kuu kukagua timu kabla ya mchezo wa
fainali kuanza,nyuma yake ni muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa
Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa
Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous
Coertz. |
|
Mashabiki wakifuatilia kwa ukaribu michuano hiyo. |
|
Muasisi
wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya, Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus
Mabula akizungumza na mashabiki wengi waliofurika katikauwanja wa
Nyamagana kushuhudia fainali hizo, ambapo hadi mwisho timu ya kata ya
Mkolani waliibuka Mabingwa kwa kuifunga Mirongo Fc 2-1. Katika Picha
anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (wa pili toka
kushoto) Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa (kushoto) na Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz (kulia). |
|
Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa naye alipata nafasi ya kuzungumza na wana Mwanza. |
|
Meneja
wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz naye alipata nafasi ya kuzungumza
ambapo aliwateka mashabiki kwa kuitumia vyema lugha ya kiswahili. |
|
Kundi la sanaa Bujora Dancing Group lilisababisha burudani nyingine ya mvuto. |
|
Burudani ilikolea macho mbeeeele kwenye tukio. |
|
Kila mtu na nafasi yake macho kwenye mchezo. |
|
Mkolani Fc wakitoka kushangilia goli la kwanza lililofungwa kipindi cha pili na Siraji Juma. |
|
Hii
ni moja kati ya zawadi za mshindi wa kwanza ambapo mbali ya kupata
Kombe, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, na medali ya dhahabu vilevile
bingwa wa michuano hiyo aliondoka na Bajaji hili lenye tahamani ya
shilingi milioni 4.5 |
|
Mkolani Fc wakishangilia bao la pili na la ushindi lililofungwa na Paul Godfrey. |
|
Mashabiki
wa Mkolani wakiwa wamembeba kocha wa timu yao mara baada ya mchezo
kumalizika wakiwa na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mirongo Fc. |
|
Zawadi ikiwa chini ya ulinzi. |
|
Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ni David Albert. |
|
Wafuatiliaji aka mashuhuda. |
|
Mwamuzi
Bora wa Mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ni David Albert,
akishangilia mara baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi laki mbili,
aliyekabidhi ni diwani wa Kata ya mirongo mhe. Mkama. |
|
Meneja
wa SBC watengenezaji wa vinywaji vya Pepsi Nilolous Coertz (Kushoto)
akimkabidhi fedha taslimu shilingi laki mbili na kiatu cha dhahabu
mfungaji bora wa mashindano Paul Godfrey wa Mkolani Fc aliye kuwa na
magoli nane (8) |
|
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida akikabidhi kombe la mshindi wa tatu kwa timu ya Sokoni Fc. |
|
Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa
akikabidhi kombe kwa washindi wa pili wa Pepsi Kombe la Meya 2014 timu
ya Mirongo Fc, ambapo pia aliwakabidhi kitita cha shilingi milioni mbili
taslimu. |
|
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi funguo na
vidhibitisho vyote vya zawadi ya gari la mizigo Bajaji kwa ajili ya
kuanzisha ujasiliamali, na mpokeaji ni Nahodha wa timu mabingwa Mkolani
Fc Meck Lymo. |
|
Wacha shangwe zitawale. |
|
Mabingwa Mkolani Fc. |
TIMU
ya Kata ya Mkolani FC imeibuka mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014
baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1 juzi katika mchezo wa
fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Awali
katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00
mchana kwa timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0na kuibuka
mshindi wa tatu wa michuano hiyo huku magori ya Sokoni yakifungwa na
Joseph Mwajalila dakika 33 kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51na
kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.
Fainali
hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi
Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa,
muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus
Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama
cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA,
Nasibu Mabrouk.
Ndikilo
amesema mashindano hayo yamewezesha vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo
ni vyema sasa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakawatumia vijana
walionesha uwezo kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la
Mbeya.
“Ni
bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda
ikatinga ligi kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu
ya Mbeya City FC inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa
huu za Toto FC na Pamba FC zimeonekana kuishiwa mbinu na kufanya vizuri
ili kurejea ligi kuu,”alisema.
Katika
mchezo huo mkali wa vuta ni kuvute kilishuhudia timu hizo zikienda
mapumziko zikiwa hazijafungana na kipindi cha pili mchezaji Siraji Juma
aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la pili likifungwa
na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira ulioelekezwa
langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo wadau wa
michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitangazwa kuwa mabingwa kwa
kuinyuka Mirongo Fc bao2 - 1.
Mashindano
hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza
vinywaji vya Pepsi (SBC), Ndikilo alikabidhi bingwa timu ya Mkolani FC
zawadi ya kombe, fedha tasilimu Sh milioni 1.5, medali ya dhahabu na
Bajaji ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili
alinyakuwa Sh milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.
Timu
ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha tasilimu Sh
milioni 1, medali ya shaba na kombe dogo, mfungaji bora Paulo Godfrey
akiwa na bao nane na kunjinyakulia kiatu cha dhahabu na Sh laki mbili,
mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance ilichukuliwa na David Albert na
kupata Sh laki mbili huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata Nidhamu bora
na Sh laki mbili.