MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 5, 2014

Picha: Uhusiano na Shilole umemsaidia Nuh Mziwanda kukuza jina lake

   925366_1521228058089857_22294318_n
Mwaka 2013 ni watu wachache tu waliokuwa wakilifahamu jina la Nuh Mziwanda kwakuwa alikuwa msanii mchanga anayetafuta nafasi yake kwenye muziki wa Tanzania. Wimbo wake ulioanza kumtambulisha uliitwa ‘Otea Nani’ ambao ulipata nafasi kiasi kwenye vituo vya redio. Lakini jina la muimbaji huyo lilikuja kuwa kubwa zaidi baada ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Shilole, uhusiano ambao umekuwa wa wazi katika mitandao yao ya kijamii. Kuonesha kuwa ana mapenzi ya kweli kwa Shilole ambaye ni mama wa watoto wawili, Nuh alijichora tattoo mkononi yenye
jina la Shilole.
Shilole pia aliamua kumpa shavu mpenzi wake kwa kuonekana kwenye video ya wimbo wake ‘Msondongoma’ na hivyo kumwongezea wigo zaidi. “Yeye ndo Mama watoto Mungu akijaalia,” aliandika Nuh kwenye picha ya Shilole aliyoiweka kwenye akaunti yake mtandao wa Instagram yenye followers zaidi ya 19,000.
 10611070_522648794547653_399585963_n
“Ukichagua kitu roho yako inapenda raha sana.sasa kwa mfano mimi Mziwanda nna haja gani ya kucheat wakati mtoto ana kila kitu, kiukweli napenda mke wangu alivyojaa jaa mie hoooooi,” aliandika kwenye picha nyingi ya Shilole.
10601700_856408051043973_284670286_n
Naye Shilole kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo akiwa na Nuh Mziwanda aliandika, “Ilove my baby,” kudhihirisha upendo wake. Hakuna shaka kuwa uhusiano huo umemwezesha Nuh Mziwanda kukuza jina lake na ameutumia vizuri kujitambulisha zaidi