Hapa wanafunzi hupata Fursa ya kujipatia Ice Crem ili kulainisha koo wakati wa kwenda nyumbani.
Mapema mwaka huu kabla ya Michango mbalimbali
kusitishwa katika shule hiyo kutokana na malalamiko ya wazazi, shule
hiyo kwa kushirikiana na wazazi walichanga fedha ambazo ziliweza
kusaidia katika kufikisha huduma ya Umeme shuleni hapo ambapo lengo
lililopo ni kuwa na darasa la Kompyuta kwa ajili ya kufundishia somo la
TEHAMA.
Aidha
tofauti na Shule nyingine ambazo zimekuwa zikionekana kukabiliwa na
uhaba wa vyoo, kwa upande wa Shule hiyo ya Bujora hali inaridhisha
kutokana na namna ambavyo shule hiyo kwa kushirikiana na wazazi
ilivyokuwa ikijitahidi kutatua mahitaji yake kupitia michango
mbalimbali, kabla ya michango hiyo kuzuiliwa ambapo kutokana na
kukosekana kwa michango hiyo hali imeanza kusababisha baadhi ya shughuli
kukwama.
|