Mgeni
rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja kuhudhuria maadhimisho hayo na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi (wa pili kulia), Kamishna
wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala (katikati) na Kamishna wa Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania , Bw. Ali Rajab (kulia)
pamoja na viongozi wengine taasisi ya watu wenye ulemavu wa ngozi
(Albinizim). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu
WAKATI
Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali duniani
kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye
misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani
Duniani wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya
albino nchini.
Akimwakilisha
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika adhimisho lililofanyika viwanja
vya Mnazi mmoja leo Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
mkazi wa UNDP nchini Alvaro Rodriguez, alisema ili kudumisha amani kuna
mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa kutambua chanzo cha migogoro
inayosababisha msuguano mkubwa katika jamii na kukosekana kwa amani.
Alisema
amani ina maana kubwa kwa jamii na ndio maana Umoja wa mataifa miaka 13
iliyopita iliamua kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kushawsihi makundi
yanayosigana kupata nafasi ya kuzungumzia na kuona maana ya amani.
Alisema
pamoja na kuwepo kwa hatua kubwa tangu kupitishwa kwa azimio la Umoja
wa Mataifa la kuadhimisha amani, safari ya kufikia amani ni ndefu na ili
kufanikiwa pande zote ni lazima kwenda hatua kwa hatua kwa
kushirikiana.
Alisema
mafanikio ambayo yamepatikana ni pamoja na UN kufanikiwa kufundisha
kada ya habari juu ya uandishi katika mazingira tete na kusaidia
majadiliano ya kitamaduni yanagusa masuala ya amani.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (katikati) akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kwa
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini
Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay.
Aidha
alisema kwamba wanafanyakazi na Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha
kwamba wanastawisha mipango yote inayolenga kuzuia ghasia na kuboresha
mipango inayoimarisha amani.
Akihutubia
bada ya mashuhuda kuzungumzia hali ya tishio la amani nchini Tanzania
hasa la kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi
albino, Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa aliipongeza serikali ya
Tanzania kw ajuhudi zake za kuimarisha amani katika kanda ya maziwa
makuu na kushiriki katika operesheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa
ziliziolenga kuleta hali bora zaidi ya maisha kwa watu wanaoishi katika
hekaheka za kivita.
Akiwa
na mwezi mmoja tangu awalisili nchini mwakilishi huyo wa Umoja wa
Mataifa nchini amesema kwamba anatarajia kuendelea kuunga mkono juhudi
za serikali na wananchi wa Tanzania kuhakikisha taifa la Tanzania
linaendelea kuwa na amanai.
Wakati
Mwakilishi huyo amesema kwamba watu wengi duniani wanawaonea gere
wananchi wa Tanzania kwa amani wlaiyonayo, mwakilishi wa Under the Same
Sun, Vicky Ntetema ametaka kupitiwa upya kwa sheria ya uchawi ya mwaka
1928 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002 ili kukabiliana na mauaji ya
albino nchini ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na waganga wa
kienyeji.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akisalimiana na Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid meza kuu.
Alisema
sheria hiyo ina mwanya mkubwa wa wauaji kucheza nayo na kusababisha
sehemu kubwa ya kesi zilizopo kushindwa kuwatia hatiani wahusika.
Alisema wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu mauaji ya albino na ukataji wa viungo umeongezeka.
Tanzania
ikiwa ni miongoni mwa nchi 25 za afrika zinazofanya ukatili dhidi ya
walemavu wa ngozi, toka mwaka 2006 watu 74 wameuawa, 56 wamenusurika na
11 wameongezewa ulemavu huku makaburi 18 ya albino yakinajisiwa kwa
kufukuliwa.
Watu
wa kituo cha haki za binadamu wamesema pamoja na kuwepo na matukio 120
ya ukatili dhidi ya albino kesi 11 tu ndio zilizofikishwa mahakamani
huku tano zikiwa zimekatiwa hukumu ambazo hazijaridhisha.
Vicky
alisema katika matukio yote hayo chanzo ni ushirikina lakini kutokana
na kukosekana zimeshindikana kuzimaliza zinavyotakiwa.
Brass
band ya jeshi la Magereza ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya
kimataifa ya amani wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam wakati wa maadhimisho hayo jana.
Vicky
aliitaka jamii kuwalinda albino kwani serikali pekee haiwezi kufanya
kitu chochote huku akisema kwamba hesabu ya albino mmoja katika kila
wananchi 1,400 haiwezi kulindwa kwa dhati na serikali kutokana na
idadi ya polisi kutokua sawa na wananchi.
Aidha
alishauri serikali kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika kabla ya
kuingia mahakamani ili waweze kusimulia vyema kadhia zao na pia
wasiangushwe na wanasheria ambao wanatumia udhaifu wa kisheria kuwatoa
watuhumiwa hatiani.
Pamoja
na Vicky Ntetema kushawishi wananchi kulinda albino na kuwafichua
wauaji Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya ameitaka serikali
kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata utulivu wa kutosha kuendelea
na shughuli zaka na kuhimiza mahakama kutenda haki.
Aliwakumbusha
wananchi kama alivyosema Sydina Omar kwamba kila mmoja ataulizwa
amefanya nini kukomesha madhila katika jamii wakati wa kiama na kusema
serikali isipowajibika itasema nini na wananchi nao pia watajibu nini.
Pichani
ni baadhi wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu
wa ngozi (Albinism) wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja huku
wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha amani
nchini na kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana
jijini Dar.
Alisema
amani hailetwi kama mvua , inatafutwa na kusema watu wasipotafuta amani
na kuhakikisha amani inakuwapo itakuwa shida kubwa kwa taifa hili
ambalo miaka yote limeogelea katika bahari ya amani.
Aliwasihi waumini wa Kiislamu na wananchi wengine kuhakukisha kwamba amani inakuwa ajenda ya kudumu kila wanapokutana pamoja.
Katika
maadhimisha hayo ambapo wananchi walianza maandamano shule ya Uhuru
Mchanganyiko hadi viwanja vya Mnazi mmoja, mgeni rasmi Waziri wa Afya na
Ustawi wa jamii Dk Seif Rashid alisema serikali imejipanga kuhakikisha
inakomesha mauaji ya albino na kuwataka wananchi kuisaidia kwa kutokuwa
waoga kutoa ushahidi na pia kuwaripoti watuhumiwa.
Alisema
kauli mbiu ya mwaka huu ya haki ya amani kwa watu wote, komesha mauaji
ya albino inahamasiaha umma wa Tanzania kulaani,kukemea na kukomesha
mauaji kwani yanakwenda kinyume na katiba ya Tanzania ya mwaka 1977
ibara ya 14 ambayo inaeleza kwamba kila mtu ana haki ya kupata hifadhi
katika jamii.
Aidha
waziri alitaka kutekelezwa kwa agizo lake kuhusu tiba mbadala na za
asili na kusema serikali itaendelea kulinda amani na kutoa ulinzi kwa
wathirika.
Meza kuu ikipoeka maandamano ya siku ya kimataifa ya amani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi akitoa
neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Mh. Seif Rashid (wa pili kulia).
Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez, Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala,
Balozi wa Uturuki nchini, Mh. Ali Davutoglu.
Mgeni
rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid, akisoma hotuba kwenye maadhimisho
ya siku ya kimataifa ya amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisoma
ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kwenye
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akipongezwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu
baada ya kusoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akisoma risala
yake kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya, akizungumza kwenye maadhimisho
hayo ambapo alilaani vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
(Albinizim) na kusema kuwa watu wote wanaoshiriki katika mauaji hayo
kamwe hawatoiona Pepo ya Mwenyezi Mungu.
Balozi
wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba
wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani
duniani.
Baadhi ya wadau kutoka taasisi na asasi mbalimbali nchini walioshiriki kwenye maadhimisho hayo.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania
(THBUB), Bi. Mary Massay akitoa nasaha kutoka kwa Tume hiyo, ambapo
alitoa rai kwa mtu yeyote yule ambaye ana malalamiko au matatizo katika
Haki za Binadamu anakaribishwa kwenye tume hiyo kwa ajili kupata msaada
wa kisheria.
Shuhuda
aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote
miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya
meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja
vya Mnazi mmoja.
Mke
wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada
ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa
mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa
anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke
wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi
mmoja jijini Dar.
Kwa matukio zaidi ingia