KUNDI maalufu la ngoma asili la Utandawazi Theater Group ‘Matwigachallo’ jioni
ya kesho wanatarajiwa kuwasha moto wa aina yake kwenye tamasha la
Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, lililoanza Septemba 22
mwaka huu kwenye viunga vya chuo hicho
NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa tamasha hilo, Abmic am Bafadhil ‘Bura’ alieleza
kuwa, kundi hilo ambalo kwa sasa limejizolea umaalufu mkubwa ndani na
nje ya Tanzania, linatarajiwa kutoa burudani ya ngoma za asili sambamba
na watoto wadoigo wanaotia fola kwa sasa katika sanaa hiyo ya utamaduni,
Watoto wadogo Gozibet Bwere (4) na Nyambuli Aginess Muganga (5).
Na
kuongeza kuwa, watoto hao wamekuwa maalufu kwa sasa hasa katika sherehe
za Kitaifa na Kimataifa kwa kupata kuonyesha uweo wao hivyo kwa uwepo
wao kwenye tamasha hilo, itatoa fursa kwa watu mbalimbali kuwaona.
Mbali
na kundi hilo la Utandawazi, pia kutakuwa na Umoja Culture Flying Carpet
ambao wataonyesha michezo mbalimbali ya sarakasi, ngoma, muziki na
michezo mingine kibao.
Aidha,
Jumamosi kutatanguliwa na mahafali ya 25 ya Chuo hicho huku wahitimu wa
37 wakitarajiwa kutunukiwa vyeti vyao, ambao Wanawake 11 na wanaume 26.