ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA MLALO
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa
kata ya Sunga.Kinana ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kata ya
Sunga,jimbo la Mlalo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa
Sunga ambapo alisisitiza kuwa matatizo mengi yanayowakabili wananchi
hayo yapo kwenye uwezo wao na wilaya kwani majibu yapo hapo hapo na
kuwaambia wananchi hao kuchagua viongozi waadilifu.
wananchi
wakifuatilia kwa umakini mkutano wa hadhara wa CCM Jimbo la Mlalo
ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia umati wa
watu.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Sunga .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Ndugu Twaha
Amir Hamza aliyekuwa akiuliza maswali juu ya matatizo ya mipaka kati ya
kijiji cha Sunga na Kwentungi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye kata ya Sunga.Katibu Mkuu wa CCM ameanzisha utaratibu wa
kuwasikiliza wananchi kwenye mikutano yake ya hadhara ambapo amekuwa
akipata maswali, ushauri au maoni ambayo pia hupatiwa majibu na Viongozi
husika.
Umati wa wakazi wa Sunga uliofurika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wasanii
wa kata ya Sunga wakifanya igizo lao baada ya Viongozi kumaliza hotuba,
wasanii hao wasanaa ya vichekesho wanafahamika kwa jina la K Square
Komedi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kijiji cha
Kwekangaga ikiwa siku ya pili ya ziara yake katika wilaya Lushoto ambapo
alishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo
la ofisi ya tawi la Kwekangaga ambayo imesema ujenzi wa ofisi hiyo
ungegharimu shilingi milioni 45 za kitanzania ,Katibu Mkuu aliigomea
taaraifa hiyo baada ya kupata ukweli kuwa ofisi hiyo ingegharimu
shilingi milioni nne na nusu tu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Kwekangaga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akisikiliza kwa makini
baadhi ya maswali kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la
Mlalo,Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangamana mwisho kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe
waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo la Mlalo uliofanyika kwenye kata ya
Lukozi wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa
kata ya Lukozi wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya shule
ya sekondari Mtumbi ambapo aliwaambia ni muhimu sana wananchi kushiriki
katika maendeleo yao kwani hakuna mtu kutoka nje anaweza kuwaletea
maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia Wazee wa kijiji cha Sunga
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia wananchi mkono
wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara kijiji cha Sunga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa eneo la mkutano Sunga.
Wananchi wa Sunga wakifuatilia mkutano wa Kinana.
Nape Nnauye akiwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara kata ya Sunga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusomba kifusi
wakati wa ujenzi wa maabara wa shule ya sekondari Mtumbi
picha habari na JIACHIE BLOG/WAMBURABABU BLOG