MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 7, 2014

AIRTEL YAANDAA UZINDUZI WA AIRTEL MUSIC TRACE KESHO COCO BEACH

Anethy Muga meneja masoko wa airtel akitangaza namba itakayotumika katika mashindano ya Airtel Trace Music  kuwa ni 0901002233 PIGA, IMBA , SHINDA na AIRTEL.
Kikundi cha yamoto Band wakipasha kwaajili ya kutoa burudani kesho katika viwanja vya COCO beach kuanzia saa 12 jioni wakati wa Uzinduzi wa Airtel Trace Music Stars,  Kiingilio ni BURE.
Airtel yaandaa uzinduzi wa Airtel Music Trace kesho Coco Beach
*       Njoo Coco Kesho - Yamoto band kufanya yao LIVE kesho BURE
*       Wateja wote wa Airtel na wasanii wanakaribishwa coco beach kesho
*       Airtel Trace namba sasa  iko wazi  kushiriki - PIGA, IMBA,
SHINDA na Airtel Trace
Kampuni ya simu za mkononi Airtel kesho inawatangazia wateja wake, wasanii na wanamuziki kuwa yale mashindano yanayotoa fulsa kwa wenye vipaji ya Airtel Trace yanaziliwa rasmi kesho katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es saalam  kuanzia saa 12 jioni Uzinduzi huu utawashirikisha wasanii Wakali nchini akiwemo Ommy Dimples pamoja na kundi zima la ya YAMOTO BAND kwa burudani kabambe kwa umati utakao jitokeza hapo kesho katika viwanja hivyo Akitoa maelezo kuhusu uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga alisema "tunawakaribisha wateja wetu, wapenzi wa muziki na watanzania kwa ujumla katika viwanja vya coco beach kesho jumatano ili kushiriki
pamoja nasi katika kusherehekea uzinduzi huu rasmi na kuanza safari ya kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Tanzania.

Airtel kupitia Trace Music Star inatoa nafasi kwa wapenzi wa muziki na waimbaji chipukizi kupata dili poa kabisa kwa kurekodi akapela zao
kupitia  simu zao za mkononi kwa kipaga na kuimba kaktika namba 0901002233 na hatimae kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo kuingia katika kinyanganyiro cha kuwa super star na mshindi wa Airtel Trace wa Afrika. Sambamba na hilo tunapenda kuwatangazia watanzani kuwa namba yetu ya
kukuwezesha kuwa mshindi ya 0901002233 sasa iko wazi, hivyo wanaweza kurekodi na kutuma nyimbo zao sasa .
kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.tracemusicstar.com