Mwanamke mmoja aliyekuwa amesafiri kwenda Kusini mwa Bara
Asia, alishtuka alipogundua kuwa mdudu anayeitwa Kaka au 'Leech' kwa kimombo na
ambaye hunyonya damu alikuwa anaishi katika pua lake.
Mdudu huyo alikuwa na urefu wa nchi 3. Mwanadada huyo
aligundua uwepo wa mdudu huyo katika pua lake baada ya kurejea kutoka katika
safari yake ya bara Asia.
Daniela Liverani, mwenye umri wa miaka 24, kutoka
mjini
Edinburgh, Scotland, amekuwa akivuja damu kutoka katika pua lake kwa wiki
kadhaa.
Hata hivyo alidhani labda mshipa mdogo wa pua lake ulikuwa
umepasuka baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki.
Bi Liverani alikuwa bafuni wiki jana Alhamisi alipogunduya
mdudu huyo kwenye pua lake alipoona kitu kikionekana kikisonga songa katika pua
lake.
Wahudumu wa hospitali, walitumia vifaa vidogo kumuondoa
mdudu huyo kutoka katika pua la Daniela.
Bi Liverani anaamini kuwa mdudu huyo aliingia katika pua
lake alipokuwa safarini Vietnam au Cambodia lakini hata alipohisi kitu
kikitembea kwenye pua lake alidhani labda ilikuwa damu iliyokuwa imeganda.
''Mimi nilidhani tu ilikuwa damu iliyokuwa imeganda,kwenye
pua langu,'' alisema Daniela.
Wakati Bi Liverani alipoingia bafuni ndipo mdudu huyo alioenakana
kwa haraka kwa sababu ya mvuke uliotokana na maji moto ambayo yaliwezesha mdudu
huyo kuteleza.
Hata hivyo alipogundua mdudu huyo alikwenda hadi hospitalini
ambako mdudu huyo alitolewa kwenye pua la mwanadada huyo.
''Madaktari walifanya kazi nzuri sana, ninawapongeza, kwa sababu sio kawaida kwao kuona kitu kama hiki kila siku,'' alisema Liverani.CHANZO BBC