amini usiamini bila sababu yyte ya maana watanzania ndo walikuwa wa kwanza kuanza kumsema kuwa hajui kuvaa, nani alimchagua , hajui kiingereza mpaka kufikia kumuigiza!!! Walisahau hata watu maruufu kama Messi na wengine wengi hawajui kuongea kabisa lugha hiyo..
Baada ya kifo chake watanzania hawahawa wakaanza kusema alikuwa nguli aliyetuwakilisha vizuri nje ya nchi na kulia sana!!!kumbe wakati akiwa hai tulikuwa tunamshusha chini..
Miaka mitano baadae Tanzania imempata mtu anayeiwakilisha vizuri nje ya mipaka na kuitangaza vizuri nchi yake..
Pasipokuwa na sababu za msingi (chuki binafsi tu)anapangiwa njama za kuzomewa na kuabishwa katika ardhi ya nchi yake ambayo kwa namna moja au nyingine kuna watu wameifahamu sababu yake!! Ukiuliza sababu za wengi wao kumchukia ni mafanikio yake lakini hata kama humpendi mtu hivi ndo hadi umzomee kwa kiasi kile !!!
leo na kesho naye huyu akitoka utaskia hawahawa waliokuwa wanamzomea wanaanza kusema jamaa alikuwa anatuwakilisha vizuri sana , ametutangaza sana kimataifa!! lakini Watanzania wenzake ndio vinara wa kumuangusha..
Si lazima kila mtu ampende Diamond ila kutumia nguvu kubwa sana kumuangusha mtu ni ishara ya uwoga na Roho ya kimaskini...
Nimeamini ""maisha bila unafki hayaendi"