Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya
Bunge la Katiba, Andrew Chenge amesema Katiba inayopendekezwa imebeba
asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko
ya Katiba.
Chenge alitoa kauli hiyo jana mjini
Dodoma alipokuwa akihitimisha michango ya hoja za wajumbe wa Bunge hilo
na kamati waliyoitoa wakati wa kuhakiki Rasimu ya Katiba hiyo.
“Bunge hili limeboresha Rasimu ya Katiba
vizuri sana. Rasimu hii imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya
Tume ya Jaji Warioba (Joseph) na nyie wajumbe mmeboresha kwa asilimia 25
tu,” alisema Chenge.
Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG), aliwataka wajumbe na wananchi wasidanganywe na
tafsiri zinazotolewa pembeni baada ya Mahakama kutoa hukumu yake.
Katika hukumu iliyotokana na kesi
iliyofunguliwa na mwandishi wa habari, Saed Kubenea, Mahakama ilitamka
kuwa Bunge la Katiba lina mamlaka ya kuboresha na kurekebisha rasimu ya
Tume.
habari na udaku special