Stori: Mwandishi wetu
MSHIRIKI wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Feza Kessy, amemtaka mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kuachia ngazi kama kweli madai dhidi yake yanamgusa nafsi yake.
MSHIRIKI wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Feza Kessy, amemtaka mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kuachia ngazi kama kweli madai dhidi yake yanamgusa nafsi yake.
Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Feza Kessy.
“Yeye ndiye anajua ukweli, arudishe kiroho safi, tumche Mungu, katika
maisha haya, hasa katika tasnia ya burudani, watu wengi sana
wanadanganya, huenda alifanya hivyo bila sisi kujua nia yake, na
ninaomba pia kama atafanya hivyo, watanzania tumsamehe,” alisema Feza,
ambaye pia alishinda taji la Miss Dar City Center na Miss Ilala mwaka
2005.
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Sitti aliyeshinda taji hilo mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es Salaam, ameibua mjadala mkubwa katika jamii, kufuatia
madai kuwa alidanganya umri wake, kwani wakati akiwa ukumbini
kujitambulisha, alidai kwamba ana umri wa miaka 18, ambao unapingwa na
wadau wa kada mbalimbali.