Hivi
karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth
Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye
kusisimua iitwayo 'MAPENZI YA MUNGU' ambapo moja kati ya washiriki
katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa
Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.
Filamu ya 'Mapenzi ya Mungu' ni moja ya filamu ambayo Lulu
ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya
wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika
kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na
muongozo anaopewa.
Filamu ya 'Mapenzi ya Mungu' itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.