MANGULA, NAPE WAONGOZA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU
Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akihutubia Vijana wa Vyuo
vya Elimu ya juu kwenye kongamano la Vijana lililofanyika Mlimani City
jijini Dar Es Salaam.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia Vijana wa CCM kutoka
vyuo Vikuu mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuadhimisha Kumbukumbu ya Baba
wa Taifa uliofanyika Mlimani City.
Nasra Khalfani akipokea kadi yake ya uanachama wa CCM
Vijana wakila kiapo cha uanachama wa CCM
Justin
Mushi akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula na kutangaza kujiunga rasmi CCM.
(Picha na Adam Mzee )
Katibu
Mwenezi wa CCM Tawi la Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Rehema Akikweti akisoma salaam za ufunguzi wa mkutano wa Vijana wa Vyuo
Vikuu wa CCM kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa.
Sehemu ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakisikiliza mada mbali mbali
Mwenyekiti wa UVCCM tawi la chuo Kikuu cha Dar es Salaam Theodora Malata akisoma risala ya Umoja wa Vijana wa Elimu ya Juu.
Katibu
Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania
Ndugu Christopher Ngubiagai akihutubia wakati wa kongamano hilo.
CCM Oyee!
Sehemu ya wanafunzi wa Elimu ya Juu wakisikiliza kwa makini mada mbali.
Wanafunzi
wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City kwenye mkutano wa
Vijana wa Vyuo Vikuu wa CCM kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa
Taifa.
Zeyana
Mohamed Haji Katibu Uchumi na Fedha Mkoa wa Vyuo Vikuu Zanzibar
akizungumzia kuboreshwa kwa Elimu ambayo itakomboa Watanzania.
Gulatone Masiga akizungumzia ubora wa Rasimu iliyopendekezwa na BMK dhidi Rasimu ya 2 ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Steve
Nyerere akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo alisema wakati umefika
kwa wasanii wa kitanzania kula milo mitatu kutokana na kukumbukwa
kwenye Katiba iliyopendekezwa.
Raymond Mweli kutoka chuo Mzumbe akizungumzia falsafa za Mwalimu Nyerere juu ya Katiba ya CCM.
Wanafunzi wakirekodi matukio kwa kutumia simu zao.