Oct 21, 2014
MSANII YP AFARIKI DUNIA
Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.
Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo
na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.
“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.
“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”
Global Publishers tunatoa pole kwa familia ya , ndugu jamaana marafiki, Bwana ametoa , Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.