MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 8, 2014

Nay wa Mitego adai ‘stunt’ ya kumwagia maji mashabiki sio agizo la mganga

Nay wa Mitego akiwamwagia mashabiki waji
                                           Nay wa Mitego akiwamwagia mashabiki maji

  Kama utakuwa unafuatilia show za Nay wa Mitego, utakuwa umeshuhudia akiwamwagia maji mashabiki wake chupa mbili mpaka tatu. Kitendo hicho kimewafanya baadhi ya watu wahoji lengo la ‘stunt’ hiyo.

Nay ameiambia Bongo5 kuwa kufanya hivyo ni kuwatia mzuka mashabiki wake na sio kama wengine wanavyotafsiri kuwa ni agizo la mganga. Rapper huyo amesema katika maisha yake hajawahi kwenda kwa mganga.
“Nilijua watu wataanza kuzungumza kuhusu yale maji ambayo nayatumia. Kitu ambacho ninaweza nikasema yale ni maji ya kawaida, sijui ni nini kimenijia kichwani, nikaamua nitumie maji na ninashangaa tu huwa nikitumia maji kuwamwagia watu wanakuwa kama wanapagawa hivi! Mzuka unakuwa juu zaidi yaani sijui ni kwanini inakuwa hivyo. Nimesikia hilo suala, sifanyi hivyo ili kutimiza agizo la mganga na maji ambayo huwaga nayatumia ni yale ambayo tunawekewaga kwaajili ya kunywa. Sijawahi kwenda kwa mganga wala sina chale niliyochanjwa ili muziki wangu u-shine,” amesema Nay.

PICHA NA BONGO 5