Amiri
Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa
maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya
kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana Jumamosi Oktoba 18, 2014. Maafisa
wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku
kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania
iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani
Arusha.
Rais
Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi
ofisa kadeti Yusup kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika
kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko
Monduli jana.Rais
Joseph Kabila wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Mwamtemi baada
ya kuibuka mwanafunzi bora katika mafunzo ya porini wakati wa hafla ya
kutunuku kamisheni baada kumaliza mafunzo ya kundi la 54/13 DRC
yaliyofanyika Chuo cha kijeshi monduli leo.Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa
hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la
54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha.Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakisimama kikakamavu wakati
nyimbo za taifa za nchi hizo zikipigwa wakati wa hafla ya kuhitimu
mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC
yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha.(Picha na Fred Maro