Aidha John Tungaraza ambaye ni Meneja
wa Tigo Kanda ya Ziwa amesema kupitia mpango huu Kampuni yake
ikishirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani,
imeahidi kuandaa siku maalum kwa madereva hao wa Bodaboda mkoa wa Mwanza
ambapo watapatiwa semina maalum itakayolenga kuboresha uendeshaji wao
kuwa salama barabarani, kuwaepusha na ajali zinazozuilika, sambamba na
kutoa leseni bure (zitakazo kuwa zimelipiwa na Tigo) kwa madereva
watakao fuzu vyema mafunzo yatakayotolewa. HABARI NA GSENGO BLOG MWANZA | |