Washindi wakiendelea kujichukulia zawadi zao toka meza kuu, ambapo michezo mbalimbali ya kuburudisha na kuimarisha afya ilihusishwa kama vile Kuvuta kamba, Kukimbiza kuku, Mpira wa miguu, Mpira wa kikapu, Riadha na mingine mingiya ubunifu alimuradi tu kuweka hamasa ya wadau kuipa kipaumbele michezo. |
Tigo mpira wa kikapu na morari yake... |
Basket ball aka Mpira wa kikapu ulihusisha watu wa jinsi zote ambapo kulikuwa na ushindani wa hali ya juu toka kwa makampuni alikwa kama vile Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mwanza (MWAUWASA), Gold Crest Hotel na Mwanza Satelite, Haya ni moja kati ya makampuni yanayo pokea huduma za MALIPO YA BAADA (Post Paid) toka TIGO ambapo kampuni inatoa idadi ya wafanyakazi na namba zao ambapo wanapata huduma mwezi mzima kisha malipo yanafanywa mwisho wa mwezi na kampuni iliyopewa huduma. Humo ndani wafanyakazi kikundi wao kwa wao huwasiliana bure bila gharama yoyote ya malipo bila kuchajiwa hata senti. |
Michezo ni urafiki michezo udumisha upendo. |
Mashabiki nao walikuwa na ligi zao katika kushangilia. |
Ushangiliaji na maubunifu yake ...hapo vipi? |
Mtanange wa soka ukiendelea katika uwanja wa TTC Butimba jijini Mwanza. |
Timu zinaenda mapumziko. |
'KAZI NA DAWA' Wakati michezo mbalimbali ikiendelea huduma mbalimbali za haraka za mawasiliano zilikuwa zikitolewa ndani ya viwanja hivi, kama vile kujisajili na Tigo Pesa, Line mpya, Vocha, Malipo kwa huduma mbalimbali na kadhalika. |
Wiki ya huduma ya mteja. |
Pozi la wadau. |
'Misosi time' |
'Kachumbari kujisevia' |
Mara baada ya maadhimisho kumalizika wadau walipeana namba za mawasiliano kisha kila mmoja akaishika njia yake |