Mratibu wa Bima ya Elimu ya
Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya
hundi kwa bwana Kennedy Kaupenda kushoto
kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. Picha zote na Mpigapicha Wetu.
TAASISI ya kifedha
ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni
tatu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy
Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.
Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.
Mwanafunzi wa MUCE, Kennedy
Kaupenda kushoto, akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi yake ya Sh Milioni 3
kutoka kwenye Bima ya Elimu inayoendeshwa na Bayport. Kulia kwake ni Mratibu wa
Bima hiyo, Ruth Bura.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima ya Elimu inayotolewa na Bayport Tanzania,
Ruth Bura, alisema Kaupenda alitajwa kama mnufaika kwa mzazi wake aliyefariki
Dunia, hivyo waliamua kumtafuta kwa ajili ya kumpatia mafao yake kwa ajili ya kuendelea kupata elimu bila vipingamizi vyovyote.
Alisema huduma
hiyo ina vipengele vine ambavyo ni Bronze, Gold, Silver na Exucutive, huku
akisema kuwa makato ya kila mwezi ya Bronze ni Sh 2,500, ambapo fao lake ni Sh
Milioni 3, wakati makato ya Gold ni Sh 6,250, huku fao lake likiwa ni Sh 7,500,000.
Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania
kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo
ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake.
Mratibu
wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura, kulia akizungumza
jambo baada ya kumkabidhi Kaupenda hundi ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye
huduma hiyo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kukamilisha ndoto za elimu
kwa uwapendao.
“Pia tunacho
kipengele cha Silver ambapo makato yake kwa mwezi ni Sh 3,800, huku mteja
akilipwa fao la Sh Milioni 4,500,000 na kipengele cha Executive kikihusisha
makato ya Sh 9,000 na kumpatia mteja fao la Sh 10,800,000, huku tukiamini kuwa
huduma hii ni sehemu ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanawawekea ulinzi wa elimu
watoto wao na yoyote wanayemchagua wao,” alisema Ruth.
Akizungumzia fao
hilo, Kaupenda alisema hakuwa na imani kuwa angesoma vizuri baada ya baba yake
kufariki, ila baada ya kutafutwa na Bayport na kutaarifiwa juu ya mafao hayo,
amepata nguvu mpya.
Kennedy
Kaupenda akitafakari baada ya kuiona hundi iliyoandaliwa kwa ajili yake
kutoka Bayport Tanzania juu ya fao la Bima ya Elimu.
“Nasikitika sana
baba kwa kunificha juu ya kujiunga na huduma hii sambamba na kuwa mkopaji wa
Bayport, hata hivyo namshukuru kwasababu fedha hizi zimekuja kunipa mwanga mpya
wa kuhakikisha kuwa nasoma kwa bidii, nikiamini kiasi cha Sh Milioni tatu
kitaniweka katika wakati mzuri mno,” alisema Kaupenda, huku akiwasisitiza
wazazi kujiunga kwenye huduma hiyo kwa manufaa ya familia zao.
Mbali na huduma
hiyo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, pia Bayport inajihusisha na mikopo kwa
watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, ambapo mwishoni mwa mwaka 2014
walizindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa, ambapo bidhaa za bodaboda aina ya Lifan,
Toyo na Boxer zinakopeshwa kwa wateja wa Bayport Tanzania.