MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 15, 2014

DIAMOND AWACHARUKIA BONGO FIVE KWA KUIPOTOSHA JAMII

msanii mkubwa wa bongo flava Nassib Abdul Aka Diamond Platnumz amechukizwa sana na kitendo cha baadhi ya wamiliki wa mitandao ya habari kupost habari zisizo za kweli mkali huyo wa miondoko ya Bongo flava ameipost katika ukurasa wake wa Facebook  huku akiinyoshea Team ya BONGO5.COM kidole kwa kile walichokipost juu ya mambo yasiyo ya kweli soma hapa alichokiandika diamond atika ukurasa wake wa acebook


  Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? Ningependa kutumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone.. Pia Nawasihi @Bongofive ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa, Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East Africa...kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari...Yawezakuwa mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama hizi....kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East Africa

CHANZO: https://www.facebook.com/DiamondPlatnumz255?fref=nf