Kambi kuu ya jeshi la umoja wa afrika mjini Mogadishu Somalia yavamiwa
Ripoti kutoka nchini Somalia zinasema kuwa kumetokea mlipuko mkubwa kwenye kituo kikuu cha jeshi la muungano wa Africa karibu na mji mkuu Mogadishu.
Hata hivyo hakuna ripoti zaidi lakini kunaripotiwa milipuko na milio ya risasi kutoka ndani ya kituo hicho.
Msemaji wa kundi la Al Shabaab anasema kuwa wapiganaji wake waliingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho na mapigano yanaendela.
Msemaji wa AU naye alithibitisha kuwepo kwa shambulizi hilo.