MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 15, 2014

MITIKISIKO YA PWANI YATIKISA MASHABIKI DAR LIVE

 
 Msaga Sumu akiwapagawisha mashabiki waliofurika Dar Live kushuhudia Mitikisiko ya Pwani.






 Mashabiki wakiwa wamepagawa na burudani kutoka kwa Msaga Sumu.

 Dida akikata mauno.

 Mashabiki wa Yanga wakipoza machungu yao baada ya timu yao kupigwa 2-0 na Simba

 Dar es Salaam Modern Taarab wakitumbuiza.

 Bi. Hindu na Dida wakipigana vijembe.

 Bi. Hindu akiwasalimia mashabiki wa Simba.

 Team Dida ikiwa jukwaani.

SHOO ya muziki wa taarab, maarufu kama Mitikisiko ya Pwani, inayofanyika kila mwaka jijini Dar, imefanyika kwa mara nyingine jana usiku katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar, ambapo wakali kibao wa muziki huo walipanda stejini na kukamua vilivyo.
Shoo hiyo inayosimamiwa na Times FM ikiongozwa na mtangazaji maarufu wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, Dida Shahibu, ilijaza umati wa watu hadi kukawa hapatoshi uwanjani hapo huku makamuzi yakifanywa na Jahazi Modern Taarab, East African Melody, Dar- es- Salaam Modern Taarab, Mashauzi Classic, Khadija Kopa, bila kumsahau bingwa wa vigodoro, Msaga Sumu.