TAMASHA LA TUONANE JANUARY (TUO8 JANUARY) LAFANA MJINI MOROGORO
Wasanii wa Hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Faridi Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Stamina wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la wazi la Tuo8January,hapo jana katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.
Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.
Msanii wa Bongo Fleva Estelina Sanga 'Linah', (kushoto), akitumbuiza na mmoja wa mashabiki katika tamashala la Tuonane Januari lililofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba mjini Morogoro.
Msanii wa Bongo Fleva Mwasiti Alimasi akipangawisha na mmoja wa mashabiki kwenye jukwaa la Tuo8Januari.
Shilole akipagawishi kwenye tamasha la Tuo8Januari lililofanyika katika Viwanja vya Sabasaba mjini Morogoro.
Weusi wakifanya yao kwenye Tamasha la Tuo8 Januari ,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.