Mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles (mbele aliyesimama) kutoka
Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari
Wanawake (TAMWA) akizungumza katika mjadala huo na wanafunzi.
Mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles (mbele aliyesimama) kutoka
Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari
Wanawake (TAMWA) akizungumza katika mjadala huo na wanafunzi. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nachitulo akizungumza na mwandishi wa habari hizi Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nachitulo walioshiriki katika mjadala wakiwa katika picha ya pamoja.
BAADHI
ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Msingi Nachitulo Wilayani Newala
wamewataka wazazi kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike kielimu kwani
kufanya hivyo ni kumnyanyasa mtoto wa kike kijinsia.
Wanafunzi hao walitoa kilio hicho hivi karibuni katika mjadala
uliofanyika kwenye shule hiyo uliokuwa ukijadili vitendo vya unyanyasaji
wa kijinsia na uelewa wa vitendo hivyo kwa watoto ili
kuweza kukabiliana navyo.
Mwanafunzi
Sofia Damian wa darasa la tano 'B' Shule ya Msingi Nachitulo
akizungumza katika mjadala huo aliwaomba wazazi kuacha tabia ya kufanya
ubaguzi wa kumjali zaidi mtoto wa kiume kielimu na kumsahau yule wa kike
kwani kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia.
Alisema baadhi ya wazazi eneo hilo wamekuwa wakibagua watoto kwa kumjali
zaidi wa kiume na kuwaacha wa kike ni ubaguzi mbaya. "...Kitendo cha
kufanya ubaguzi wa elimu katika familia kwa mtoto wa kike na kiume ni
unyanyasaji wa kijinsia…yaani kumpeleka mtoto wa kiume shuleni na
kumuacha wa kike nyumbaji hilo ni unyanyasaji," alisema Sofia Damian.
Kwa
upande wake Sharifa Bakari toka darasa la sita 'A' katika shule hiyo
alisema ubaguzi wa mtoto
wa kike umekua ukianzia ngazi za familia kwa watoto wa kike kuwa na kazi
nyingi nyumbani zaidi ya mtoto wa kiume kitendo ambacho kinatakiwa
kipigwe vita.
Mwanafunzi
wa darasa la sita 'A' katika shule hiyo, Mwanahamisi Said aliwataka
baadhi ya wazazi na walezi kuacha utaratibu wa kumlazimisha mtoto wa
kike kuolewa kwa taamaa ya mali (ndoa za utotoni), kwani kitendo hicho
pia ni ukatili wa kijinsia. "..Hata kitendo cha mtu mzima kumlazimisha
mwanafunzi kufanya naye mapenzi ni ukatili wa kijinsia," alisema
Mwanahamisi.
Akizungumza
mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles kutoka Kituo cha Usuluhishi
(CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA)
aliainisha matukio ya ukatili wa kijinsia yanayowapata watoto na kutoa
elimu ya kukabiliana nayo kwao, ikiwa ni pamoja na wao kutoa taarifa
mapema sehemu husika endapo watatokewa na hali kama hizo.
Akizungumza awali kabla ya mjadala huo, Mwalimu wa Malezi wa Shule ya Msingi Nachitulo, Blandina
Luwongo alisema shule hiyo imefanikiwa kupiga vita vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia kwa
watoto kwa kutumia mradi wa elimisha rika jambo ambalo limeondoa kabisa matukio ya mimba kwa wanafunzi.
"...Katika
shule yetu hata matukio ya wanafunzi kutiwa mimba hayapo kwa sasa baada
ya elimu ya uelimishaji rika kutolewa kwa jamii, wanafunzi na walimu
eneo hili. Hata hivyo anabainisha ili kutokomeza kabisa matukio ya
unyanyasaji elimu ya kukabiliana na vitendo hivi kwa jamii haina
budi kutolewa kiufasaha na kuacha kujikita kwenye adhabu kwa wakosaji."
Anasema Bi. Luwongo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com