Wananchi wa kangae A Nyakato Mwanza wakitengeneza barabara
Wananchi kata ya Kangae ''A'' nyakato Jijini mwanza mapema leo
wameshirikiana na kuamua kutengeneza barabara iliyokuwa imeshindikana
kutengenezwa kwa muda mrefu kwani wamekuwa wakipata shida kubwa ya
usafika hasa wakati wa masika na mvua kubwa zinaponyesha. wananchi hao
wa kata ya kangae wamefanya zoezi hilo chini ya uongozi wa mwenye kiti
wao na kamanda wa usalama Polisi jamii Bw. Tumbo ndozero amabe amekuwa
akiongoza zoezi hilo kwa umakini zaidi.
Wananchi kata ya Kangae ''A'' nyakato Jijini ameiambia blog hii kuwa wao hawako tayari kupata shida na kuisubiri serikali kuja kuwatengenezea barabara wao wataendelea tu siku serikali ikiwa tayari basi watakuja wamalizie sehemu itakayokuwa imesali. wananchi hao wenye umoja wamejituma hatimaye wamaefanikiwa kupata barabara nzuri yenye kupitisha magari na pikipiki kwa urahisi zaidi na hivyo wao wenyewe wamefurahia umoja wao.
muonekanao wa barabara kabla ya kufanyiwa matengenezo na wanachi wa kata ya kangae A nyakato
wananchi wakipeana ushirikiano zaidi kutengeneza barabara
wakina mama nao walikuwepo kutengeneza barabara maana wao ndio wenye mahitaji makubwa zaidi ya barabara hususani wakati wanapokuwa wajawazito huitaji barabara zilizo nzru kuepuka mitikisiko ya tumbo
barabara imeanza kuonesha muonekano mzuri na watu wako bize na kazi kamakawaida
wazee nao hawakuwa mbali waliamka na kuchapa kazi
mwenyekiti akiongoza wanchi wake katika harakati za utengenezaji wa barabara
barabara yetu hiyoooo sasa twaeza kuitumia vizuri sana
mitaro ikirekebishwa vizuri kwaajili ya kupitisha maji
tumeanza kuitumia barabara