MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 11, 2014

WATANZANIA WAASWA KUENDELEA KUSAIDIA SEKTA YA MICHEZO NCHINI

unnamed
WaziriwaHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wadau wa michezo ya Ngumina na Karate wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Zantel Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose.
unnamed1 
Ulingo wa kisasa kwa ajili ya Mchezo wa Ngumi uliotolewa kama msaada na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL na kupokelewa naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara leo jijini Dar es Salaam.
unnamed3 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akijaribu baadhi ya vifaa vya mchezo wa ngumi (Gloves) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose na katikati yao mwenye suruali nyekundu ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Bw.Lukelo Willilo.
unnamed4Afisa Mtendaji Mkuu wa ZANTEL Pratap Ghoe akisalimiana na Bingwa wa mchezo wa ngumi Tanzania Bondia Francis Cheka (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Ulingo wa Kimataifa kwa ajili ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Picha zote na: Frank Shija, WHVUM